Pengine umejaribu kuangalia series ya Game of Thrones lakini umeshindwa kuielewa kwa sababu mbalimbali.
Huu ni utangulizi wa baadhi ya mambo yaliyotokea katika dunia ya ‘Ice And Fire. Mengi utayosoma hapa kwenye utangulizi hayaonekani kwenye GOT, ni historia tu inayosimuliwa na watu mbalimbali ndani ya series lakini tumeanza kuoneshwa kwa uchache pia kwenye House of the Dragon.Ni muhimu kuijua ili uweze kuelewa baadhi ya matukio utakayo yaona yakiwa yanatokea au yanaongelewa.
Let’s go…
Katika dunia ya kufikirika, ni mabara mawili tu ndiyo yanajulikana, Westeros na Essos.- Westeros (West/magharibi).
- Essos (East/mashariki).
![]() |
| Westeros & Essos |
Mabara haya mawili yanatenganishwa na bahari nyembamba (Narrow Sea). Westeros ni Bara ambalo miaka 12,000 iliyopita halikuwa na watu wa kawaida bali walikuwepo watu wafupi wanaoitwa ‘Children of the Forest’ wakati ‘Essos’ ilikuwa na watu wa kawaida.
![]() |
| Children of the Forest |
Westeros ni bara kubwa. Watu wa Essos walianza kuja Westeros kutafuta makazi mapya miaka 12,000 iliyopita. Kila walivyokuwa wanafikia sehemu walikuwa wanaanzisha utawala wao.
Kusini ambayo ni sehemu kavu walianzisha Dorne, Magharibi walianzisha The Reach na The Rock, Kaskazini walianzisha The North na tawala nyingine nyingi lakini kulikuwa na ugomvi na ‘Children of the Forest’ uliopelekea kutokea kwa ‘White Walkers.
Miaka 8,000 iliyopita The North waliokuwa chini ya utawala wa Starks waliamua kujenga ukuta mkubwa kuwazuia White Walkers wasije tena kwao, huo ukuta unaitwa “The Wall” Una urefu wa futi 7,00 na unatoka ukingoni mwa bahari ya mashariki hadi magharibi.
Kwenye The Wall kuna walinzi ambao mara nyingi huwa wanapelekwa wahalifu waliokubuhu kama sehemu ya adhabu kwao, wakati mwingine watu hujitolea tu kwenda kuwa walinzi.
Ukikubali kiapo cha kuwa mlinzi wa ukuta huruhusiwi kuoa, kuwa na watoto (kama wakati unaapa’ ulikuwa huna) wala kujihusisha na mambo yoyote ya utawala wa nchi. Ukitoroka adhabu yake ni Kifo.
Kama nilivyosema lengo la kujengwa kwa ukuta lilikuwa ni kuwazuia White Walkers wasivuke kuja kwa watu lakini White Walkers wamepotea na hawajaonekana kwa takribani miaka zaidi ya 1,000 sasa.
Kuna watu ambao hawakupenda kutawaliwa, wapo kaskazini mwa ukuta, ni wengi na ni makabila mbalimbali, huko kaskazini mwa ukuta kuna baridi kali na huwezi kulima chochote, hali hiyo inawalazimu wakazi wa huko waishi kwa kuiba, Je wanaiba wapi?
Walikuwa wanavuka ukuta kwa kupanda juu wanavamia vijiji wanaiba kisha wanarudi tena kaskazini. Watu wa Westeros wanawaita watu hao ‘Wildings’. Na kwa sasa kazi kubwa ya walinzi wa ukutani ni kuzuia Wildings wasivuke kuja kuiba vijijini.

| Wildings |
Hali ya hewa; Kuna majira ya Joto (summer) na majira ya baridi (winter).”
Tofauti na dunia yetu ambapo majira yanakuwa yanachukua kipindi cha miezi kadhaa, huko majira yanachukua kipindi cha miaka.
Miaka 300 iliyopita alikuja jamaa mmoja anaitwa Aegon Targaryean akiwa na dada zake wawili aliambatana na ‘Dragons’ ambao waliwatumia kwenye vita. Aegon alifanikiwa kuvunja tawala zote za Westeros kisha akajitangaza yeye kuwa ndiye mfalme wa bara zima.
Aegon Targaryean na dada zake (ambao aliwaoa) wakatawala Westeros yote. Wakati Aegon Targaryean na dada zake wanakuja kulikuwa na falme 7 kwenye bara la Westeros.
Tofauti na dunia yetu ambapo majira yanakuwa yanachukua kipindi cha miezi kadhaa, huko majira yanachukua kipindi cha miaka.
Mfano: Tanzania; majira ya mvua yanaanza Novemba hadi Mei. Na majira ya kiangazi yanaanza Juni hadi Oktoba.Westeros: majira ya joto yanaanza mwaka 2000 hadi mwaka 2008, majira ya baridi yanaanza 2009 hadi 2014, kisha yanakuja tena majira ya joto.
Miaka 300 iliyopita alikuja jamaa mmoja anaitwa Aegon Targaryean akiwa na dada zake wawili aliambatana na ‘Dragons’ ambao waliwatumia kwenye vita. Aegon alifanikiwa kuvunja tawala zote za Westeros kisha akajitangaza yeye kuwa ndiye mfalme wa bara zima.
Aegon Targaryean na dada zake (ambao aliwaoa) wakatawala Westeros yote. Wakati Aegon Targaryean na dada zake wanakuja kulikuwa na falme 7 kwenye bara la Westeros.
![]() |
| Muonekano wa falme kaba ya Aegon Targaryean kutawala. |
1. The North iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Stark
2. The Mountains and the Vale iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Arryn
3. The Isles and the Rivers iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Hoare
4. The Stormlands iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Durrandon
5. Dorne iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Martell
6. The Reach iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Gardener
7. The Rock iliyokuwa inatawaliwa na familia ya Lannister
Baada ya Aegon kuwashinda watawala wa falme hizi aliunda tawala ndogo 9 ambazo zilikuwa kama majimbo na kuweka wawakilishi wake (Wardens).
Baadhi ya watawala kama Starks wa the North hawakutaka kupigana na Aegon ili kulinda watu wao, baadhi walipigana na wakashindwa vibaya kama Hoare na baadhi walifanikiwa kumshinda kama Martell wa Dorne (baadae walijiunga na utawala wake kwa makubaliano).
![]() |
| Baada ya Aegon kuanza kutawala |
Hizi ndiyo tawala 9 alizoanzisha Aegon Targaryean;
1. The North
– Warden wake ni familia ya Stark
– Makao makuu – Winterfell
– Nembo: Mbwa mwitu
2. The Riverlands
– Warden wake ni familia ya Tully
– Makao makuu – Riverrun
– Nembo: Samaki
3. Iron Islands
– Warden wake ni familia ya Greyjoy
– Makao makuu – kisiwa cha Pyke
– Nembo: Pweza mkubwa (kraken)
4. The Vale
– Warden wake ni familia ya Arryn
– Makao makuu ni The Eyrie
– Nembo: Kipanga (Falcon)
5. Westerlands
– Warden wake ni familia ya Lannister
– Makao makuu – Casterly Rock
– Nembo: Simba
6. Dorne
– Warden wake ni familia ya Martell
– Makao makuu – Sunspear
– Nembo: Jua na mkuki
7. The Reach
– Warden wake ni familia ya Tyrell
– Makao makuu – Highgarden
– Nembo: Ua la rose
8. Stormlands
– Warden wake ni familia ya Baratheon
– Makao makuu -Storm’s End
– Nembo: Swala mwenye mapembe yenye matawi
9. Crownlands
– Haina warden, mtawala wake ni mfalme ambaye anatawala bara zima.
– Makao makuu yake ni jiji la King’s Landing ambalo pia ndiyo makao makuu ya ufalme wa bara zima.
– Nembo: Dragon mwenye vichwa vitatu
Ndani ya tawala hizi kubwa kuna familia nyingine ambazo zinakuwa zinatawala eneo fulani. Familia hizo zinakuwa na bendera zake na nembo zake pia lakini zinakuwa tiifu kwa utawala wa warden.
Aegon Targaryean alizaa na dada zake na ukoo wao uliendeleza utamaduni huo kwa muda mrefu ili kuifanya damu yao isichanganyike na watu wengine, Utawala wa familia ya Targaryean ulidumu kwa miaka karibia 3,00.

.jpeg)

.jpg)

0 Comments